1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres asema MONUSCO inakaribia kuondoka Kongo

12 Agosti 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema ujumbe wa kulinda amani wa umoja huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaingia katika awamu yake ya mwisho.

https://p.dw.com/p/4V5om
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres Picha: Eskinder Debebe/UN Photo/Xinhua/IMAGO

Guterres hata hivyo ametoa tahadhari huwa hali katika taifa hilo lenye mzozo imezorota kwa kasi.

Kupitia ripoti yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Guterres alitoa tathmini ya kina juu ya machafuko katika taifa hilo na kutangaza mipango ya kuuondoa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO, kwa njia ya haraka lakini isiyoyumbisha usalama.

Ripoti hiyo ya kurasa 15 imeonesha kuwepo kwa ongezeko la mivutano na hali mbaya ya kiutu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wakati maelfu ya raia wakilazimika kuyahama makazi yao.

Taarifa hiyo imeeleza pia kuwa, unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto umeongezeka mara mbili kutoka mwaka 2021 hadi 2022. Maeneo yalioathiriwa zaidi na mzozo huo yametajwa kuwa ni Kivu Kaskazini  na Ituri,