1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano na vurugu vyaendelea New Caledonia

Saumu Mwasimba
14 Mei 2024

Hali ya maandamano ya vurugu imekuwa ikiendelea katika kisiwa cha New Caledonia ambacho ni himaya ya Ufaransa kilichoko nje ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4fqD1
Neukaledonien Noumea | gewaltsame Proteste
Picha: THEO ROUBY/AFP

Watu wanaounga mkono uhuru wa kisiwa hicho kilichoko katika eneo la Kusini mwa bahari ya Pacific, Mashariki mwa Australia, na wanaotaka kujitenga na Ufaransa, wamekuwa wakiandamana kupinga hatua za serikali ya mjini Paris, za kutaka  kufanya mageuzi ya katiba,ambayo yatawapa maelfu ya raia wa Ufaransa wanaoishi katika kisiwa hicho haki ya kupiga kura na kuipa nafasi nchi hiyo kuwa na ushawishi zaidi wa kisiasa kwenye kisiwa hicho.

Ripoti zinasema, tangu jana Jumatatu maduka chungunzima na magari yalitiwa moto huku kukiripotiwa pia kutokea uporaji na watu kukamatwa.

Shule na shughuli za huduma za umma zimesitishwa kwa siku kadhaa.Kisiwa cha New Caledonia ni eneo muhimu la kimkakati la shughuli za kijeshi na lenye madini ya Nickel.