1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

semenya kubeba bendera ya Afrika kusini

27 Julai 2012

Caster Semenya atapeperusha bendera ya Afrika Kusini katika michezo hii ya Olimpiki. Hayo yalidhihirishwa wakati wa matangazo yaliyofanywa mjini Johannesberg huko Afrika Kusini.

https://p.dw.com/p/15fhL
Aug 19, 2009; Berlin, GERMANY; Caster Semenya (RSA) takes a victory lap after winning the women's 800m in 1:55.45 in the 12th IAAF World Championships in Athletics at Olympic Stadium. Photo via Newscom Picture-Alliance
Caster SemenyaPicha: picture-alliance / Newscom

Semenya mwenye umri wa miaka 21 alipewa fursa hiyi hivi karibuni. Mwogeleaji Cameron Van der Burgh na mrukaji Khotso Mokoena pia walikuwa katika ile orodha ya watu waliochaguliwa na kamati ya Olimpiki.

Semenya alisema kuwa ni fursa ya kiheshima kwake kufanya alichokiita kitu kikukubwa cha kubeba bendera ya taifa kwa niaba ya timu itakayoiwakilisha Afrika Kusini.

Msimamizi mkuu katika kamati ya Olimpiki ya Afrika Kusini, Tubby Reddy alisema kuwa walikuwa wakimfikiria pia mwanariadha Pistorius ambaye atafanya jambo la kihistoria kwa kuwa kuwa mlemavu wa kwanza kukimbia katika michezo ya Olimpiki baada ya kutajwa katika dakika za lala salama kuwa ni miongoni mwa watakaojiunga timu ya Afrika Kusini katika mashindano hayo.

Tubby Reddy alisema kuwa kulikuwa na wanariadha wachache waliotarajia kuibeba bendera hiyo mjini London kwa hivyo walimchagua Semenya. Aliongeza pia kuwa amekuwa mshindi wa dunia na wanatarajia kuwa atashinda medali ya dhahabu katika Olimpiki mwaka huu. Tubby aliongeza kuwa iwapo wangemchagua Oscar Pistorius basi kungetokea maswala mengine.

LONDON, ENGLAND - JULY 26: Hera the Harris's Hawk with handler Andrew Watson ahead of the London 2012 Olympics at the Olympic Park on July 26, 2012 in London, England. (Photo by Jeff J Mitchell/Getty Images)
michezo ya olimpic 2012Picha: Getty Images

Semenya, ambaye ni mshindi wa zamani katika mbio za mita 800 na aliyeshinda medali ya fedha mwaka uliopita hakuhudhuria sherehe ya kuwaaga rasmi timu ya kuiwakilisha taifa hilo kwa vile alikuwa Monaco ambako anafanya matayarisho ya mwisho kabla ya mashindano ya Olimpiki huko London. Aliikubali fursa hiyo ya kubeba bendera ya Afrika kusini kupitia ujumbe uliorekodiwa. Natalie du Tout, mwogeleaji wa Olimpiki ndiye alieibeba bendera hiyo mwaka 2008 katika mashindano ya michezo ya Beijing.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Semenya kushindana katika Olimpiki. Miaka mitatu iliyopita alikumbwa na tetesi za kuthibitiwa kwa jinsia yake kufuatiwa na ushindi wake mkubwa mjini Berlin, Ujerumani. Semenya alilalamika kuwa kutakiwa kwa thibitisho la jinsia yake sio muhimu na kuwa itakuwa uvamizi wa faragha yake.

Alitengwa kwa miezi 11 wakati shirika la IAAF ilikuwa ikihakiki majaribio ya jinsia yake na kukubaliwa kurudi katika mashindano mwaka 2010 lakini hangeweza kushindana kwa sababu ya maumivu ya mgongo. Mwaka uliopita alimaliza wa pili katika mbio za mita 800 kule South korea licha ya kuhangaika na maumivu hayo.

Aidha, Semenya aliwaambia waandishi wa habari wa Ulaya kuwa jinamizi hilo ameliacha nyuma na kuwa ana matarajio ya kushinda dhahabu katika Olimpiki ambayo akipata atakitunukia Nelson Mandela ambaye ni mwanasiasa maarufu wa Afrika kusini.

Semenya anakumbuka wakati wake wa kwanza kukutana naye Nelson Mandela alikuwa msichana mdogo tu. Lakini Nelson Mandela alikuwa na imani kwake. Kwa hivyo chochote anachokifanya ni kwa ajili yake Mandela kwa vile yeye humtia moyo.

Caster Semenya ambaye rekodi yake ya muda mfupi zaidi ni dakika 1.59 na sekunde 18 amewai kushindwa mara 5 na mshindi wa Olimpiki ya mwaka 2008 na Mkenya Pamela Jelimo. Lakini anasema kuwa anaangalia mbele. Kila mwaka anazidi kuwa mwanariadha bora kwa hivyo mashindano haya yatakuwa ya nia thabiti kwake.

Mwandishi : Trizer Ochieng/AFPE
Mhariri: Sudi Mnette