1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania:Kuchukua hatua kukabiliana na hali ngumu ya maisha

George Njogopa5 Mei 2022

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amelazimika kuitisha kikao cha dharura na mawaziri wake ili kujadili namna ya kuikwamua hali mbaya ya ugumu wa maisha inayosababishwa na kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta.

https://p.dw.com/p/4Aqz6
Tansania Vizepräsident Kassim Majaliwa
Picha: DW/S. Khamis

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amelazimika kuitisha kikao cha dharura na mawaziri wake ili kujadili namna ya kuikwamua hali mbaya ya ugumu wa maisha inayosababishwa na kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta.

Katika mkutano wake wa dharura na mawazirikadhaa Waziri Mkuu, Kassaim Majaliwa amesema serikali haiwezi kufumba macho wakati wananchi wake wanaendelea kutaabika.

"Sisi kama nchi tunafanya nini ili kukabiliana na hali hii katika nchi" Alisema waziri mkuu katika kikao chake na jopo lake la mawaziri ili kutafuta suluhu kuleta ahueni ya masiha kwa raia wa taifa hilo la Afrika Mashariki.

Soma Pia:Tanzania: Wananchi walalamika kukosa bidhaa muhimu

Bei ya mafuta katika baadhi ya maeneo sasa imefikia zaidi ya shilingi 3,200 za Kitanzania kutoka kiwango cha awali kilichokuwa 2,700.  

Kutokana na hali hiyo wananchi hadi sasa hawajajua ni namna gani watapaswa kujifunga mkanda kutokana na kuendelea kupanda kwa gharama za maisha huku sekta kama za usafiri pamoja na chakula ikionekana kuzidisha zaidi ugumu wa maisha.

Bunge lajadili ugumu wa maisha kwa dharura

Vita vya Urusi na Ukraine inatajwa ni moja ya sababu ya kupanda kwa bei ya mafuta, lakini baadhi ya wachambuzi wanasemautitiri wa tozo inaweza kuwa ni sehemu ya sababu nyingine.

Tansania Dr. Tulia Ackson
Spika wa Bunge la Tanzani Dokta Tulia AcksonPicha: Ericky Boniphace

Suala hilo la kodi nyingi zilizowekwa kwenye mafuta limekuwa moja ya mjadala mkubwa uliozuka bungeni leo wakati bunge hilo lilipoanzisha mjadala wa dhahura kujadili hali hiyo inayoendelea sasa.

Sehemu kubwa ya wabunge waliitaka serikali kuleta mpango wa dharura ili kuikwamua hali ya mambo hasa wakati ambapo wananchi wanaendelea kutaabika na hali ngumu ya maisha.

Soma pia:Bei ya Umeme nchini Tanzania

Ingawa hadi sasa bado haijafahamika ni lini serikali itauleta mpango huo wa dharura, lakini Waziri wa Nishati January Makamba akizungumza bungeni leo asubuhi, amesema serikali itazingatia hoja zote zilizotolewa na wabunge.

"kama serikali tumechukua hoja zote,tunafahamu udharura na uharaka wake" Alisema waziri makamba na kuongeza kuwa lazima uzingatiwaji wa sheria, kanuni na utaratibu katika masuala ya kodi.

Wananchi bado wametega masikio kujua namna serikali itakavyolishughulikia suala hilo huku kukiwa na wasiwasi kuwa huenda gharama za maisha zikaendelea kupanda iwapo majawabu ya suala hilo yanatakawia kuwafikia wananchi hao.

Kilio cha kupanda kwa bei za bidhaa