1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upepo mkali na mvua kubwa yashuhudiwa pwani ya Tanzania

Saleh Mwanamilongo
4 Mei 2024

Sehemu kubwa ya Tanzania imekosa umeme hivi leo wakati mvua kubwa na pepo kali za Kimbunga Hidaya zikikaribia kuipiga nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

https://p.dw.com/p/4fVlW
Umeme wakatika Tanzania wakati Kimbunga Hidaya kikikaribia
Umeme wakatika Tanzania wakati Kimbunga Hidaya kikikaribiaPicha: Hadi Mizban/AP/picture alliance

Shirika la umeme la nchi hiyo, TANESCO, lilitangaza kukatika huko kwa umeme kulitokana na hitilafu ya gridi ya umeme.

Taarifa hiyo ilitolewa leo kabla ya kukaribia Kimbunga Hidaya. Idara ya hali ya hewa nchini humo ilisema kimbunga hicho kilikuwa kinaelekea pwani ya Tanzania.

Huduma za usafiri wa maboti baina ya mji mkuu wa kibiashara, Dar es Salaam, na visiwa vya Zanzibar ulisitishwa wakati Kimbunga Hidaya kikikaribia pwani ya Afrika Mashariki kikiwa na kasi ya kilomita 120 kwa saa, na huku kukiwa na upepo mkali.

Mamlaka nchini humo zilionya kwamba wananchi wanapaswa kuchukuwa hadhari kubwa wakati huu kimbunga kikikaribia.